• Middle East
  • North Africa
  • Global
  • Business
  • Finance
  • Technology
  • Press
  • About Us
    • Press Release Distribution Services
    • Submit Press Release
    • Contact Us
Submit Press Release
Search
Close
Search
Close
Home North Africa

Mradi wa Maji waiimarisha ahadi yake ya kusafisha maji katika Kaunti ya Vihiga, Kenya

admin by admin
January 26, 2023
in North Africa
The Water Project Deepens its Commitment to Clean Water to Vihiga County, Kenya
Share on FacebookShare on Twitter


Regional Director of The Water Project Humphrey Buradi and His Excellency The Governor of Vihiga County, Dr. Wilber Khasilwa Ottichilo at MOU signing. Humphrey Boradi et son excellence le gouverneur du comté de Vihiga, le Dr. Wilber Khasilwa Ottichilo lors de la signature du protocole d'entente.
Regional Director of The Water Project Humphrey Buradi and His Excellency The Governor of Vihiga County, Dr. Wilber Khasilwa Ottichilo at MOU signing.







KAUNTI YA VIHIGA, MAGHARIBI MWA KENYA – (AFRICA NEWSWIRE): Mnamo tarehe ishirini Januari, Kaunti ya Vihiga Magharibi mwa Kenya ilitia saini Mkataba wa Maelewano (MOU) na The Water Project, Shirika lisilo la Kiserikali lenye makao yake makuu Marekani linalojenga miradi ya maji endelevu ili kuleta maji safi, salama na ya kutegemewa kwa jamii za Kaunti ya Vihiga.

“Kutiwa saini kwa MOU kunawakilisha mwendelezo wa uhusiano dhabiti wa kikazi kati ya Serikali ya Kaunti ya Vihiga na The Water Project, tukitambua dhamira yetu ya pamoja ya kutoa maji kwa jamii za Vihiga, kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu wa miundombinu ya WASH, na kujenga na kubadilishana maarifa miongoni mwa watendaji wa sekta,” alieleza Emma Kelly, Meneja Programu katika The Water Project.

Ahadi ya The Water Project Magharibi mwa Kenya ilianza zaidi ya miaka kumi na miwili iliyopita. Shirika hilo, likiongoza na kufanya kazi kupitia wafanyakazi wa ndani na washirika wa mtandao, ikiwa ni pamoja na Western Water and Sanitation Forum (WEWASAFO) na Friends of Timothy Foundation (FOTF), linashirikiana na jamii kufuatilia na kudumisha karibu miradi elfu moja mia tatu ya maji inayotekelezwa kote kanda. Miradi hiyo ya maji ina faida kwa takriban watu lakini nne na hamsini.

Mheshimiwa Gavana wa Kaunti ya Vihiga, Dkt. Wilber Khasilwa Ottichilo alisema, “Maji ni mojawapo ya ajenda zetu kuu. Ushirikiano na The Water Project unatazamia kutekeleza afua za kutoa huduma za maji na usafi wa mazingira kwa wakazi wa Vihiga.”

Mradi wa Maji unafanya kazi ili kufikia upatikanaji kamili wa maji na usafi wa mazingira katika maeneo yake ya huduma, kuanzia na kaunti ndogo ya Hamisi huko Vihiga. Shirika linatekeleza programu za maji na usafi wa mazingira kupitia uchimbaji wa visima, ukarabati wa visima, ulinzi wa vyanzo vya asili, uvunaji wa maji ya mvua, utoaji wa vifaa vya vyoo, na uhamasishaji wa usafi kwa jamii na taasisi zilizo hatarini.

Mnamo mwaka wa 2022, The Water Project ilikamilisha zoezi la kuchora ramani kubainisha vituo elfu ishirini na sita, ishirini na moja vya maji vya umma na vya kibinafsi, katika majimbo mbalimbali ya matumizi, ili kuelewa wigo halisi wa kazi inayohitajika kufikia huduma ya msingi ya maji kwa wakazi wote. Shirika litachapisha matokeo ya kazi hii baadaye mwakani kadri mipango ya muda mrefu ya eneo inavyozingatiwa.

“Tuna furaha na unyenyekevu kuweza kuendelea na kuimarisha kujitolea kwetu kwa watu wa Magharibi mwa Kenya tunapotoa maji safi, salama na ya kutegemewa kwa wale ambao leo wanateseka bila sababu,” alisema Peter Chasse, Rais na Mwanzilishi wa The Water Project.

Kaunti ya Vihiga iko katika eneo la Magharibi mwa Kenya. Kaunti hii ina kaunti ndogo tano: Luanda, Emuhaya, Hamisi, Sabatia, na Vihiga.

The Water Project, shirika lisilo la faida la Marekani, ambalo lina makao makuu ya kikanda Kakamega, Kenya, linafungua uwezo wa kibinadamu kwa kutoa miradi ya maji ya kutegemewa kwa jamii za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Taarifa zaidi zinapatikana kwente tovuti thewaterproject.org

 

Courtney Field
Mkurugenzi wa Masoko,
The Water Project
603-369-3858
Courtney@thewaterproject.org

Taarifa hii kwa vyombo vya habari inatolewa kupitia Africa Newswire™ (www.africanewswire.net) – huduma ya habari kwa Afrika, na inasambazwa na EmailWire™ (www.emailwire.com) huduma ya kimataifa ya mtandao wa habari ambayo hutoa usambazaji wa taarifa kwa vyombo vya habari na matokeo ya uhakika™.











Source link

Tags: EmuhayaHamisiKenyaLuandaMradi wa MajiPeter ChasseSabatiaTHE WATER PROJECTVihiga
Previous Post

The Water Project Renforce son Engagement en Faveur de l’Eau Potable dans le Comté de Vihiga, Kenya.

Next Post

Bioink Market is expected to grow at a CAGR of 20.48 percent during the forecast period

RelatedPosts

BZR on Coinstore – a Significant Milestone for Bazaars
North Africa

BZR on Coinstore – a Significant Milestone for Bazaars

BZR on Coinstore Facebook Twitter Pinterest WhatsApp LinkedIn Email Reddit Bazaars, the up-and-coming crypto-based P2P marketplace, makes a...

by admin
March 24, 2023
Kaafmeem to Provide VIP Clothing for Saudi Motorsport Company during Formula1 event in KSA.
North Africa

Kaafmeem to Provide VIP Clothing for Saudi Motorsport Company during Formula1 event in KSA.

Kaafmeem selected for VIP Staff Uniforms at Formula1 Facebook Twitter Pinterest WhatsApp LinkedIn Email Reddit Local Saudi brand...

by admin
March 23, 2023
أعرب 83٪ من المسلمين عن ولعهم بالمنتجات والخدمات الصديقة للبيئة ، وفقا لاستطلاع أجرته TGM Research
North Africa

أعرب 83٪ من المسلمين عن ولعهم بالمنتجات والخدمات الصديقة للبيئة ، وفقا لاستطلاع أجرته TGM Research

TGM Ramadan Global Survey 2023 Data Pill Facebook Twitter Pinterest WhatsApp LinkedIn Email Reddit تطلق TGM إحدى الدراسات...

by admin
March 18, 2023
أوتيكو تتصدر ١٣٠٠٠ عينة بيئية تم تحليلها في ميناء تامان
North Africa

أوتيكو تتصدر ١٣٠٠٠ عينة بيئية تم تحليلها في ميناء تامان

Oteko Facebook Twitter Pinterest WhatsApp LinkedIn Email Reddit  MOSCOW, RUSSIA (ARAB NEWSWIRE) أفاد أوتيكو أن ميناء تامان قد تم...

by admin
March 9, 2023
Load More

Advertize

Latest Post

The Dhahab Sports Web 3.0 is going to be the biggest sports digital asset launching for 2023

The Dhahab Sports Web 3.0 is going to be the biggest sports digital asset launching for 2023

by admin
March 25, 2023

BZR on Coinstore – a Significant Milestone for Bazaars

BZR on Coinstore – a Significant Milestone for Bazaars

by admin
March 24, 2023

Exchange goods, vehicles, or property for crypto on Bazaars

BZR on Coinstore – a Significant Milestone for Bazaars

by admin
March 24, 2023

Kaafmeem to Provide VIP Clothing for Saudi Motorsport Company during Formula1 event in KSA.

Kaafmeem to Provide VIP Clothing for Saudi Motorsport Company during Formula1 event in KSA.

by admin
March 23, 2023

A 4-month old calf escaped a slaughterhouse and roamed the streets of Brooklyn. Now she’ll live out her days at a sanctuary.

A 4-month old calf escaped a slaughterhouse and roamed the streets of Brooklyn. Now she’ll live out her days at a sanctuary.

by admin
March 22, 2023

Live news: First Republic bosses to skip bonuses as Fitch slashes its credit rating

Live news: First Republic bosses to skip bonuses as Fitch slashes its credit rating

by admin
March 22, 2023

MENANEWS provides press release distribution services for businesses, organizations and other entities with the need to reach media outlets in Europe, Middle east and Africa (MENANEWS) Submit press release or contact us today.

Share us

Subscribe To Our Newslatter

    • Middle East
    • North Africa
    • Global
    • Business
    • Finance
    • Technology
    • Press
    • About Us
      • Press Release Distribution Services
      • Submit Press Release
      • Contact Us
    Menu
    • Middle East
    • North Africa
    • Global
    • Business
    • Finance
    • Technology
    • Press
    • About Us
      • Press Release Distribution Services
      • Submit Press Release
      • Contact Us

    Browse by Category-

    Middle-East/ North Africa/ Global/ Business/ Finance / Technology/ Press/ About Us / PR Services / Submit PR / Contact us

    © 2023 Copyright MENANEWS

    Share us

    Share on facebook
    Facebook
    Share on twitter
    Twitter
    Share on linkedin
    LinkedIn
    Share on pinterest
    Pinterest